Rais Dkt Samia kuipa NECTA mitambo ya kisasa ya uchapaji

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kutokana na kukua kwa teknolojia siku hadi siku, mitambo ya uchapishaji inapoteza ubora wake, hivyo ili kuongeza ufanisi katika Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), serikali itaongeza mitambo mitatu ya uchapishaji ambapo itaongeza mtambo mmoja mmoja kila mwaka ili baraza liendelee kuboresha huduma zake kupitia teknolojia.

Akizungumza leo katika kilele cha Maadhimisho ya Miaka 50 ya NECTA mkoani Dar es Salaam, Rais Samia ameliagiza baraza hilo kutunza vifaa na mitambo ya uchapishaji ili kuepusha serikali kuingia gharama.

"Kwa sababu tunataka ufanisi kwenye baraza la mitihani tutakwenda kuangalia katika bajeti zetu zijazo tukaangalie tuone uwezekano wa kuongeza mtambo mmoja mmoja kila mwaka," amesema Rais Samia.

No comments