Benjamin Mkapa, Uhuru vyafungwa hadi mwakani

Serikali ambayo inamiliki viwanja viwili vya michezo vya Benjamin Mkapa na Uhuru vilivyoko jijini Dar es Salaam, imevifunga kwa matumizi kupisha ukarabati mkubwa hadi utakapokamilika Oktoba mwakani.

Katika taarifa iliyotolewa muda huu, hali hiyo inatokana na uwanja wa Uhuru kubainika kutokuwa katika hadhi ya kikanuni kuweza kuruhusu michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.

Kupitia taarifa hiyo, serikali ilisema awali ilikubali timu zilizoomba kuvitumia viwanja hivyo kama.viwanja vyao vya nyumbani ziendelee kutumia huku ukarabati ukiendelea, lakini sasa imeona ni bora vikafungwa kabisa hadi ukarabati utakapokamilika.

Simba na Yanga zimekuwa zikiutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama.uwanja wao wa nyumbani katika Ligi Kuu na ile ya klabu Afrika, wakati KMC imekuwa ikiutumia uwanja wa Uhuru.

No comments