Katibu Mkuu CCM ajiuzulu
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amejiuzulu nafasi yake, siku chache baada ya barua yake ya kujiuzuru kuonekana mitandaoni na kuzusha taharuki kubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi hilo la Chongolo wakati akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama chake kilichofanyika kwa siku mbili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Paul Makonda.

Post a Comment