MCHEZAJI WA GHANA ALIYEKUFA KWA TETEMEKO UTURUKI KUZIKWA LEO

H
Image caption: Jeneza la Mchezaji soka wa Ghana Christian Atsu, likiwasili kwa ajili ya shughuli ya mazishi mjini Accra Ghana

Mchezaji soka wa Ghana Christian Atsu, ambaye alifariki baada ya tetemeko la ardhi kuikumba Uturuki anazikwa leo Ijumaa katika nchi yake ya asili Ghana.

Atsu alipatikana akiwa amefariki baada ya tetemeko la ardhi kuangusha nyumba ya gorofa ambamo alikuwa anaishikusini mwa Uturuki . Alikuwa akiichezea klabu ya soka ya Hatayspor.

g
Image caption: Atsu alifariki katika tetemeko la adrhi lililoikumba Uturuki

Shuguli ya mazishi yake ambayo yamesaidiwa na taifa la Ghana inafanyika katika mji mkuu Accra.

Maelfu ya waombolezaji wamefika katika eneo la mazishi kutoa heshima zao za mwisho kwa Christian Atsu, katika mazishi yanayofanyika kwa utamaduni wa Ghana.

Hizi ni baadhi ya picha za mazishi ya Christian Atsu, zilizochukuliwa na mwandishi wa BBC wa Ghana Thomas Naadi:

B

No comments