KARDINALI PENGO AZURU KABURI LA JPM CHATO
Katika kuadhimisha miaka miwili ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Joseph Magufuli, aliyekuwa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Kardinali Policarb Pengo, amezuru kaburi lake lililopo kijijini kwao Chato.
Pengo ambaye alikuwa mmoja ya viongozi wa dini walioheshimika kwa Rais Magufuli, katika ziara hiyo aliungana na baadhi ya wana familia akiwemo Mama Janeth Magufuli.

Post a Comment