MAHAKAMA YAAMURU MUSIBA KUMLIPA BERNARD MEMBE SHILINGI BILIONI SITA
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imemuamuru
Mmiliki wa Gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba kumlipa aliyekuwa Waziri wa
Mambo ya Nje, Bernard Membe kiasi cha Sh.Bilioni 6 kama fidia ya kumchafua
kupitia vyombo vyake vya habari.
Hukumu hiyo ni ya shauri la kesi namba 220 ya mwaka 2018 na
imetolewa na Jaji Joacquine De Mello ambapo amesema mbali na mambo mengine
Musiba amlipe Sh.Bilioni 6 Membe, pia inatoa zuio la kudumu la kutomkashifu
Membe au kusema uongo dhidi yake na kulipa gharama za kesi.
Mahakama imesema Sh.Bilioni 5 ni fidia ya hasara halisi na
Sh. Bilioni 1 hasara ya jumla, katika kesi hiyo Membe alimshtaki Musiba,
Mhariri wa gazeti la Tanzanite na wachapishaji wa gazeti hilo ambapo
aliwadai Sh. Bilioni 10 kwa kumchafua.
Musiba katika kesi hiyo alishtakiwa kwa kumtuhumu Membe kuwa
anamhujumu Rais John Magufuli asitekeleze majukumu yake ya kuwaletea
wananchi maendeleo huku akidai kwamba mbinu mojawapo ya kukamilisha hujuma hizo
ni maandalizi anayofanya kugombea urais mwaka 2020 kupitia CCM

Post a Comment