DPP AMFUTIA MASHTAKA MHADHIRI CHUO KIKUU KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Mkurugenzi wa Mashitaka ya jinai nchini l (DPP)amemfutia
Mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyokuwa yakimkabili Mahakamani mhadhiri wa Chuo
kikuu cha SAUT tawi la Arusha, Subilaga Masebo na wenzake wanne.
Akiwasilisha maombi ya kuondoa shtaka hilo, mwendesha mashtaka
wa serikali Lusiana Shaban ameiambia mahakama ya wilaya Babati Mkoani Manyara
,upande wa jamhuri haina Tena Nia ya kuendelea na shtaka hilo lililofunguliwa
dhidi ya washtakiwa hao.
"Mheshimiwa hakimu ,kesi hii ilikuja Kwa ajili ya
kusikilizwa lakini upande wa jamhuri unawasilisha Mbele Yako maombi ya
kuliondoa shauri hilo mahakamani"alisema Shaban.
Alisema tunaomba kufanya hivyo kupitia kifungu Cha 91(1) Cha
Sheria ya makosa ya jinai, sura ya 20 ya mwaka 2019.Tunaliondoa shauri hili Kwa
hiyari bila kushurutishwa na yeyote.
Katika shauri hilo wengine waliokuwa wameshtakiwa ni Hilari
Mmbando,Hemed Nyokaa, Ramadhani Hasani na Ally Juma wote wakati wa wilaya ya
Babati.
Mhadhili huyo alikuwa akitetewa na wakili Kapimpiti Mgalula
wa jijini Arusha baada ya kufunguliwa kesi hiyo ya jinai namba 39/2021 katika
mahakama ya wilaya Mkoani Manyara, April 29,mwaka huu yeye na wenzake
wakikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 40
.50 yaliyokuwa kwenye gari yake.
Akisoma uamuzi wa kuondolewa Kwa shauri hilo, Hakimu wa
wilaya ya Babati Victor Kimaro alisema mahakama yake haina pingamizi na uamuzi
wa serikali wa kuondoa shauri hilo mahakamani.
Alisema washtakiwa hao Kwa Sasa wapo huru kuendelea na
shughuli zao kama kawaida ,Hata hivyo aliongeza kuwa upande wa mashtaka unaweza
kufungua upya shauri hilo wakati wowote itakapotaka.
Akizungumza nje ya mahakama wakili Mgalula alimshukuru DPP
Kwa kuwafutia mashtaka watuhumiwa wote kwani aliamini kwamba Mhadhili huyo
hakuwahi kuhusika na biashara ya mirungi ukizingatia kwamba yeye ni mhadhili wa
Chuo kikuu,taaluma inayoheshimika kwenye Jamii.
Naye Sublaga Masebo ambaye alikuwa mshtakiwa namba moja
katika shauri hilo ,alisema katika maisha yake hakuwahi kufanya biashara ya
mirungi ila kilichomponza ni kuwapatia lifti kwenye gari yake watu
wasiofahamika na baada ya kusimamishwa na askari polisi Watuhumiwa walifanikiwa
kutoroka na yeye kukamatwa ,hivyo anashukuru mahakama kwa kumwachia huru.

Post a Comment