WACHEZAJI WOTE WAZAWA KUBAKI SIMBA -GOMES

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba Didie Gomes da Rosa amesema anatamani wachezaji wote wazawa wa timu hiyo wabakie kikosini msimu ujao.
"Toka nimejiunga na Simba nimegundua kwamba wachezaji nilionao ni bora kuliko waliopo timu zingine hapa Tanzania ni kipaumbele changu kuwabakisha klabuni hapa.
Sitoruhusu mchezaji wa
kitanzania yoyote aondoke Simba ila kama anataka kuondoka au hafanyi ninavyotaka
milango iko wazi kuondoka." alisema Gomes na kusisitiza haoni kama kuna
mchezaji yoyote Tanzania ana kitu cha ziada kuwazidi wachezaji alionao pale
msimbazi.
Wachezaji wa simba wanaomaliza
mikataba yao mwishoni mwa msimu huu..
1.Ibrahim Ajibu
2.Francis Kahata
3.Miraji Athumani
4.Ally Salim
5.Beno Kakolanya
6.Gadiel Michael
Kwa upande wa Kocha wa makipa
Milton Nienov amesema kwake yeye makipa wote watatu(Salim, Kakolanya na Manula)
wabaki kikosini msimu ujao.
Gomes amesema pia bado kuna
mechi kadhaa za kucheza kwahiyo mchezaji asipocheza mechi hii anaweza kucheza
inayofuata.

Post a Comment