'Watoto hawakulala usiku kucha' - Israel kuhusu shambulio la Iran
Hadithi ya shambulio la kipekee la Iran dhidi ya Israeli ingekuwa tofauti kama matayarisho ya Israeli hayangefaulu sana. Israel inasema 99% ya ndege 300 zisizo na rubani na makombora ya baharini na ya balestiki ambayo yalikuwa yamerushwa yaliangushwa na nchi hiyo na washirika wake.
Siku ya Jumapili, Israeli iliporejea katika hali ya kawaida, hiyo ilikuwa chanzo cha sherehe - wakati kila mtu, hapa na mahali pengine, akingojea jibu mwafaka kutoka kwa Israeli.
"Nguvu za Israeli ni kwamba tuna ngao, ulinzi dhidi ya vitisho hivi," Ariel mwenye umri wa miaka 54 ananiambia, huko Jerusalem. “[Shambulio la Irani] lilitarajiwa ... Israel labda itajibu. Natumai hakutakuwa na vita”
Shambulio la Iran halikuwa jambo la kustaajabisha, kwani kwa takriban wiki mbili nchi hiyo ilikuwa imetangaza nia yake ya kujibu shambulio la anga kwenye makao yake ya kidiplomasia katika mji mkuu wa Syria, Damascus, ambalo liliua washauri kadhaa wa kijeshi, wakiwemo majenerali wawili wakuu - shambulio linaloaminika na watu wengi kufanywa na Israel.
"Tulijua kwamba Iran ingeshambulia ... Tulikuwa na wasiwasi kidogo. Lakini tunajua tuna ngao kubwa,” Einat mwenye umri wa miaka 44 anasema. "Hatutaki mambo yawe mabaya zaidi [na majibu]."
Marekani ilikuwa mojawapo ya nchi zilizosaidia katika ulinzi wa Israel, lakini maafisa wa utawala wa Biden wanasema hakutakuwa na uungaji mkono wa Marekani kwa jibu la Israel, na kwamba hatua ya Israel kwenye shambulio hilo tayari ilikuwa ushindi dhidi ya Iran.
"Ilikuwa [usiku] wa kutisha, watoto hawakulala usiku kucha, walikuja kitandani kwetu, wakalala nasi," Moran mwenye umri wa miaka 41 anasema. "Tuna jeshi lenye nguvu zaidi ulimwenguni, na tunaamini itakuwa sawa. Natamani tungeshambulia, lakini hatuwezi kwa sababu ya Marekani.
BBC

Post a Comment