Mwenyekiti CCM Pwani aongoza ukaguzi maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko Rufiji
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg Mwinshehe Mlao jana tarehe 06/04/2024ameiongoza Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani kwa kutembelea Maeneo ya Kata zilizo athiriwa na Mafuriko baada ya Mvua kubwa zinazo endelea kunyesha Wilayani Rufiji.
Mwenyekiti Mlao amewaomba wananchi kuchukua tahadhari kipindi hiki ambacho Serikali na Chama wanaendelea kuwasaidia wahanga hao.
Aidha, Mwenyekiti amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kuwafikia haraka wananchi wa RUFIJI walioathirika na mafuriko hao kwa kuwapatia Misaada mbalimbali.
Naye Mbunge wa Jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Tamisemi Mhe Mohamed Mchengerwa kwa kushirikiana na Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani wamewakabidhi Waathirika hao Magodoro na vyakula huku wakiahidi kuendelea Kuwasaidia.
CCM Mkoa wa Pwani inatoa pole kwa Wana Rufiji wa Kata 12 Kati ya 13 zilizokutwa na Mafuriko hayo.
*#Poleni Sana Wanarufiji*
*#Serikali na Chama KAZINI Kuwasaidia*
Imetolewa na
David Mramba Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo CCM
Mkoa wa Pwani

Post a Comment