Mbeya wamhakikishia Dkt Nchimbi imani yao kwa CCM



Matukio mbalimbali katika Mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili Jijini Mbeya kutokea Mkoani Songwe.

Katika mkutano huo, Wananchi wa Mbalizi wamemuhakikishia Katibu Mkuu Balozi Dkt. Nchimbi kuwa hawatayumba wala kuyumbushiwa na mtu , watu au chama chengine cha siasa tofauti na Chama Cha Mapinduzi na wana imani kubwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuomba awafikishie salamu zao za upendo kwake.

Akizungumza na maelfu ya Wananchi walijitokeza, Balozi Dkt. Nchimbi ameeleza thamani na wajibu wa mwanachama wa CCM katika Taifa.

Vilevile amesikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa maelekez ya CCM kwa baadhi ya viongozi wa serikali kushugulikia kero na changamoto ambazo hazikutatuliwa papo kwa papo kwakuwa zilihitaji maelezo na utibitisho wa kujiridhisha zaidi.

Balozi Dkt. Nchimbi ameingia Jijini Mbeya na atakuwa kwa muda wa siku 2 kuanzia leo tarehe 16 hadi 18, Salamu ziwafikie wana Mbeya wote kila kona kushiriki katika mikutano yake.

Dkt. Nchimbi ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Amos Makalla Pamoja na Katibu wa NEC - Oganaizesheni Ndugu. Issa Haji Gavu.

No comments