WALIMU MKOANI MOROGORO WAMPONGEZA DK.MOHAMED MWAMPONGWA KWA KUTUNUKIWA SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA (PhD)


Na Ojuku Abraham, Dar es Salaam

Baadhi ya Walimu Mkoani Morogoro wametoa pongezi zao za dhati kwa Mwalimu mwenzao Dk.Mohamed Mwampogwa kwa hatua kubwa aliyopiga ya kutunukiwa Shahada ya Juu ya Udaktari wa Heshima (Honorary Causa) kutoka katika Chuo kikuu cha Kimataifa cha ANCC International University cha Texas USA.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mkoani Morogoro Mwl. Halidi Iddy alisema Shahada hiyo ya juu si tu imemheshimisha yeye na Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania bali imetuheshisha Walimu wote nchini na kutupa chachu ya kumbapania majukumu yetu ya kusaidia maendeleo ya taifa letu.

"Binafsi namfahamu vizuri Dk.Mwampogwa ni Mkurugenzi wetu wa Jukwaa la Wazalendo huru Tanzania ni mtu Mcheshi,mtu makini na Mzalendo anaependa kusimamia kile anacho kiamini na hata likizo ya mwezi Disemba 2023 nilikuwa miongoni mwa watu walio mpokea hapa Mkoani kwetu Morogoro,tulishauriana naye mambo mengi ya kujitolea kwa ajili ya taifa letu hivyo hatua zake ni zetu maana zinatufikirisha na kututia Moyo tutumikie vyema nchi yetu" Alisema Mwl.Halidi Iddy ambaye katika Jukwaa ni Katibu wa Elimu,Siasa na Hamasa Jukwaa la Wazalendo huru Mkoani Morogoro.

Naye Mwalimu Julieth Kimaro Anael Afisa Elimu Kata kutoka Mkoani Morogoro ambaye pia alihudhuria katika Mahafali ya Dk.Mwampogwa alisema ilikuwa ngumu tutohudhuria kwa kuwa Dk.Mwampogwa ni mtu wa watu na kuna kitu kikubwa chá kiupendo ambacho alikiwekeza kwetu Wana Morogoro na Watanzania nao ni Upendo na Uzalendo hivyo mimi na wenzangu akina Khan,Juvier na wengineo tukaona tukaweke nae Historia hii muhimu kwake Mungu ambariki sana na sisi katufunza jambo zuri sana kupitia mapambano yake.

Dk.Mwampogwa alitunukiwa Shahada hiyo na Chuo Kikuu cha ANCCIU kutokana na mchango wake wa HUDUMA aliyoitoa kwa Jamii na taifa lake na Mahafali yalifanyika siku ya Jumamosi tarehe 23.03.2024 huku Prof.Purity Gatobu kutoka Kenya ambaye alikuja kuwatunuku Shahada hizo kwa niaba ya Mkuu wa Chuo akimpongeza sana Dk.Mwampogwa na kumpa ukaribisho maalum nchini KENYA katika Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta ambapo Prof.Purity anafanyia kazi.


No comments