RC MWANZA CPA AMOS MAKALLA NA MHE MNYETI WAKUBALIANA KUPELEKA FFU SHAMBA LA MAABUKI MISUNGWI

 

Mhe Mkuu wa mkoa wa Mwanza CPA AMOS MAKALLA na Mhe Mbunge wa Jimbo la Misungwi na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti wamekubaliana kupeleka askari polisi wa kutuliza ghasia kwenye shamba la Mifugo Mabuki lililopo wilayani Misungwi.

Mhe AMOS MAKALA alipokea malalamiko hayo alipofanya ziara na kuzungumza na watumishi wa shamba hilo na watumishi wamekuwa wakipigwa na wachungaji wa Mifugo  Toka  nje ya Misungwi wanapokuja kuchunga wakiwa na silaha zenye ncha kali kama vile Visu na mapanga  na wakati  mwingine MAWE 

Kutokana na wafugaji Toka nje ya wilaya ya Misungwi kuvamia na kuchungia kwenye shamba hilo la serikali Mhe Mnyeti amekubali Mpango huo wa serikali wakupeleka askari hao ili walilinde shamba hilo kongwe lililoanzishwa na  Hayati Rais mstaafu J.K. Nyerere mwaka 1967.

Shamba hilo kwasasa Lina taasisi kubwa tatu na zinajiendesha kwa kujitegemea ikiwa zimepewa maeneo na taasisi ya shamba la Mifugo Mabuki.

Taasisi zilizopo kwasasa ni LITA CAMPUS MABUKI na TARIRI MABUKI hizi zote zinafuga Mifugo mbali mbali na kuuza Mifugo kwa wananchi wanao hitaji.

Taasisi ya tariri imejikita sana kwenye Utafiti wa Mifugo na malisho Bora huku ikiwa imefanikiwa sana kuwa na mbuzi nyingi Toka nje ya nchi pia.

Mhe Rais Dkt Samia Hassan Suluhu pia ametoa Ng'ombe zaidi ya 300  za kisasa chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Mpango wa serikali wa BBT life.

Pia kupitia Ziara ya makamu wetu wa Rais Dkt Philipo Isdory Mpango wilayani Misungwi alipiga marufuku wachungaji kuchungia kwenye shamba hilo.Na serikali kulilinda sana.

Hivyo viongozi wetu wa serikali mnatakiwa kulilinda sana shamba hili la Historia kubwa ya nchi yetu.Kwani Kuna NYATI  walio letwa na Hayati Rais mstaafu J.K. NYERERE.

Shamba la Mifugo Mabuki ni urithi wetu.Tuwarithishe kizazi chetu.


No comments