Seruikali kutoa bilioni 1.3 kujenga soko la kimataifa la Tarime
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeridhia kutoa TZS. bilioni 1.3 ili kukamilisha soko la kimataifa la mazao ya kilimo lililopo Renagwe, wilayani Tarime, mkoani Mara.
“Masoko haya tumeyajenga kila palipo na mpaka. Tumejenga Namanga, Tunduma, Kasumulo, Horohoro, Holili pamoja na hili la Tarime ambalo ni la muda mrefu, zabuni ya kulikamilisha hili na la Horohoro tayari zimeshatangazwa,”
Waziri Mkuu amesema kuwa tayari zabuni zimekwishatangazwa na kazi itaanza kabla mwezi Machi haujaisha. “Serikali inataka wakulima walitumie soko hilo kupeleka mazao yao ili wanunuzi kutoka ndani na nje ya nchi wakanunue mazao katika soko hilo.”
Ametumia pia mkutano huo kuwaagiza mameneja wa TANESCO katika mikoa na wilaya nchini wapige kambi vijijini na kutoa huduma hapohapo ili kurahisisha ulipaji wa gharama za kuunganishiwa umeme badala ya kusubiri kufuatwa makao makuu.

Post a Comment