Dani Alves: Mshtakiwa hakuniambia niache, wote tulifurahia tendo
Alves, mlinzi wa Brazil na Barcelona, ambaye kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa yupo gerezani akisubiri kesi hiyo kumalizika, aliiambia mahakama kuwa alikubaliana na mwanamke huyo kushiriki tendo hilo, kwani kabla ya hapo, walicheza wote muziki huku wakiwa na jamaa zao.
Mshtaki wake anasema mwanasoka huyo mwenye tuzo nyingi alizopata katika enzi zake za soka, alimlazimisha kufanya naye mapenzi katika klabu hiyo ya watu mashuhuri jijini Barcelona Desemba 31, 2022.
Hata hivyo, mwanamke huyo ambaye utambulisho wake umefichwa, alikiri kucheza muziki na Alves na kwamba alienda pamoja naye chooni kwa hiyari, lakini wakati akitaka kutoka ndipo alipomzuia, kumchapa kibao kabla ya kumwingilia kinguvu.
"Mimi siyo mtu wa hivyo na kila mtu anajua. Hakuniambia niache na sisi wote tulifurahia tendo," Alves aliiambia mahakama iliyofurika watu, akiwemo mkewe aliyetengana naye kufuatia kashfa hiyo, Joana Sanz.
Joana Sanz (wa pili kushoto), mke wa zamani wa staa wa FC Barcelona na Brazil Dani Alves, na mama yake Dona Lucia (wa pili kulia) wakiondoka mahakamani ikiwa ni siku ya pili ya kesi ya mchezaji huyo inayosikilizwa na mahakama jijini Barcelona.

Post a Comment