Makonda amwagiza Waziri wa Ardhi kufika jimboni Kawe kutatua mgogoro wa ardhi akiwa na Mbunge

 


Katibu wa Siasa, Itikadi, Mafunzo na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Paul Makonda amempigia simu ya moja kwa moja Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa akiwa katikam mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mpira wa Bunju Shule.

Makonda alimtaka Waziri Silaa kufika jimboni hapo ili kutatua changamopto ya migogoro ya ardhi iliyopo katika maeneo ya Chasimba, Nyakasangwe, Mbopo DDC na kuahidi kufuatilia kwa ukaribu.

Vile vile amepongeza jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Katika jitihada zake binafsi za kununua greda kwa ajili ya kutengeneza barabara Kisha akamuongeza greda 20 ili zifanye kazi ndani ya siku 7 katika Jimbo zima la Kawe chini ya TARURA.



No comments