Katibu CCM Kibaha Vijijini awaasa UWT Kibaha kuwa wamoja


Kibaha Vijijini. 

anuari 18, 2024.


Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini Ndg. Steven E. Shija ambaye ni mjumbe wa Baraza La UWT Wilaya na Mlezi wa Jumuiya za CCM, amewakumbusha Wanawake wa UWT kuwa wamoja kwa maslahi ya CCM

Amewakumbusha kujijenga kiuchumi ili kutokuwa Wategemezi kama Viongozi wa Kitaifa chini ya Mwenyekiti wake Ndg Marry Chatanda (MCC) wanavyopambana kujenga Uchumi wa UWT Taifa, na kushughurika na Mambo yanayowahusu Wanawake wote

Pia amewaagiza Madiwani wote wa UWT kuhakikisha wanaandaa taarifa za utekelezaji wa Majukumu yao kila baada ya miezi Sita na kuziwasilisha ofisi ya UWT Wilaya mapema, siyo wasubiri hadi waombwe kufanya hivyo maana huo ni wajibu wao kufanya UWT ijue wanachotekeleza katika nafasi waliyoaminiwa

Vile vile amewataka Viongozi na Wanachama wa UWT kuepukana na makundi yanayopelekea kuleta mivurugano ndani ya Chama, na amewahamasisha Wanawake wote Wilaya ya Kibaha Vijijini kujitokeza kwa Wingi kugombea bafasi mbalimbali Katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa


Imetolewa na Idara ya Siasa na Uenezi, Wilaya ya Kibaha Vijijini

No comments