DC Lushoto awasilisha taarifa ya utekelezaji Ilani kwa Kamati Kuu wilaya

DC LUSHOTO AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KAMATI KUU WILAYA


MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Mhe. Kalisti Lazaro (pichani), leo amewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Kikao cha Kamati Kuu ya Wilaya kilichofanyika kwenye Ukumbi wa CCM Wilaya ya Lushoto.

Akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili (Bumbuli na Lushoto), Wakuu wa Idara na vitengo pamoja na Wakuu wa Taasisi za Umma zilizopo ndani ya Wilaya ya Lushoto, Mhe. Lazaro aliwaeleza wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Wilaya namna ilani ya uchaguzi ya CCM ilivyotekelezwa wilayani Lushoto.

Mhe. Lazaro alisema kwamba Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Wilaya ya Lushoto imetekelezwa kwenye nyanja mbalimbali kuanzia Elimu, Afya, Kilimo, Miundombinu, Maji na Umeme huku akimshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kulete fedha nyingi za utekelezaji wa miradi wilayani humo.

Katika hatua nyingine. Kwa kauli moja Kamati Kuu ya CCM, Wilaya imeridhishwa na namna Ilani ya Uchaguzi ya CCM ilivyotekelezwa wilayani humo hivyo kwa kauli moja waliipokea na kuikubali taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kama ilivyowasilishwa na Mhe. Lazaro.

No comments