Wakuu wa shule za sekondari wachanga fedha za fomu ya Urais Samia Suluhu Hassan

 


Wakuu wa shule za sekondari nchini, wamechanga jumla ya shilingi 1,600,000 kwa ajili ya kumkabiodhi Rais Samia Suluhu Hassan aweze kuzitumia kuchukua fomu ya kugombea urais wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mweka Hazina wa umoja wa walimu hao, Zamoyoni Uzale alisema kwa sasa wanamsubiri waziri wa Tamisemi ili awape utaratibu wa namna ya kumpatia fedha hizo. Fomu ya kuwania Urais kupitia Chama cha Mapinduzi ngazi ya Urais huchukuliwa kwa shilingi milioni moja.

No comments