Mke wa mkuu wa upelelezi wa Ukraine apewa sumu, yasema Kyiv
Mke wa mkuu wa Ujasusi wa Ukraine Lt Jenerali Kyrylo Budanov, Marianna Budanova, ametiliwa sumu ya vyuma vzito, msemaji wa idara ya upelelezi ya kijeshi ya nchi hiyo ameiambia BBC Ukraine
Andriy Yusov alisema wafanyikazi wengine kadhaa shirika hilo pia walikuwa na dalili kali za sumu.Hakutaja ni wangapi.
Ripoti katika vyombo vya habari vya Ukraine hazikusema ikiwa Urusi ilidhaniwa kuhusika na shambulio hilo au la.
Hakukuwa na ishara kwamba Jenerali Budanov pia anaweza kuwa alilengwa.
Jenerali huyo, ambaye anaongoza Kurugenzi Kuu ya Ujasusi (DIU) ya wizara ya ulinzi ya Ukraine, amekuwa na jukumu muhimu katika kupanga na wakati mwingine kutekeleza operesheni kubwa za kijeshi dhidi ya vikosi vya Urusi, kufuatia uvamizi kamili wa Moscow mnamo Februari 2022.
Chanzo cha kijasusi cha Ukraine hapo awali kiliiambia BBC Bi Budanova alikuwa akitibiwa hospitalini baada ya kuugua.
Tovuti ya habari ya Babel, ambayo Jumanne ilikuwa ya kwanza kuripoti madai hayo ya sumu, ilisema Bi Budanova alipelekwa hospitalini baada ya kujisikia vibaya kwa "muda mrefu".
Ikinukuu vyanzo vya kijasusi vya Ukraine, Babel ilisema sasa anakamilisha kozi ya matibabu na hali yake itafuatiliwa na madaktari.

 
 
Post a Comment