Hivi sio vita, huu ni ugaidi, anasema Papa kuhusu mzozo wa Israel na Hamas
Papa Francis alifanya mikutano tofauti na familia za Israeli za mateka wanaoshikiliwa na Hamas na Wapalestina pamoja na jamaa zao Gaza.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki amesema mzozo wa Israel na Hamas umevuka vita, na kuwa "ugaidi", na kusisitiza kuwa "pande zote mbili zinateseka."
Akizungumza katika hadhira yake ya kila juma katika Uwanja wa St Peter's Square, muda mfupi baada ya mikutano katika makao yake, papa huyo alisema: "Wanateseka sana na nilisikia jinsi pande zote mbili zinavyoteseka."
Aliongeza: "Tafadhali tusonge mbele kwa ajili ya amani... Baraka zangu ziwaendee wote."

 
 
Post a Comment