Cristiano Ronaldo anakabiliwa na kesi ya $1bn kuhusu matangazo ya Binance

 

Mchezaji kandanda Cristiano Ronaldo anakabiliwa na kesi nchini Marekani kuhusu matangazo yake kuiuza Binance, soko kubwa zaidi la kubadilisha fedha za kielektroniki duniani.

Walalamikaji wanadai uidhinishaji wake uliwaongoza kufanya uwekezaji uliowasababishia hasara

Wanatafuta fidia ya "kiasi kinachozidi" $1bn (£790m).

BBC imewasiliana na kampuni ya usimamizi ya Ronaldo na Binance kwa maoni.

Mnamo Novemba 2022, Binance alitangaza mkusanyiko wake wa kwanza wa "CR7" wa tokeni za (NFTs) kwa ushirikiano na Ronaldo, ambazo mwanasoka huyo alisema zingewatuza mashabiki "kwa miaka yote ya usaidizi".

NFTs ni mali pepe zinazoweza kununuliwa na kuuzwa, lakini ambazo uhalisia wa kuonekana moja kwa moja - kwa maneno mengine zinapatikana kidijitali pekee. Kwa ujumla, hutumiwa kuashiria umiliki wa kitu, kama vile picha au video mtandaoni.

"CR7" inaashiria herufi za kwanza na nambari ya shati ya Ronaldo, na hutumika kama chapa katika bidhaa mbalimbali, kuanzia viatu hadi manukato, ambazo zimesaidia kumfanya kuwa mmoja wa wanariadha matajiri zaidi duniani .

Katika video ya mtandao wa kijamii akitangaza ushirikiano huo, Ronaldo aliwaambia watarajiwa wawekezaji "tutabadilisha mchezo wa NFT na kupeleka soka kwenye ngazi ya juu zaidi".


No comments