Yahya Sinwar ni nani na kwanini Israel inamsaka?

 

Israel imedhamiria "kumsaka" kiongozi wa Hamas Yahya Sinwar, ikisema anahusika na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel.

Msemaji wa jeshi la Israel, Daniel Hagari alisema kuwa Sinwar ni muuaji ambaye aliuthibitishia ulimwengu kuwa Hamas ni waovu zaidi ya ISIS baada ya mauaji ya Oktoba 7."

Afisa huyo wa Israel aliongeza: "Tutaendelea kumfuatilia hadi tumpate."


Oktoba 29, Yahya Ibrahim Al-Sanwar alitimiza miaka sitini na moja. Alizaliwa katika kambi ya wakimbizi ya Khan Yunis huko Gaza 1962.

Al-Sinwar anatoka katika familia iliyoishi katika jiji la Al-Majdal Ashkelon - kabla ya kutangazwa kuwa eneo la Israeli 1948.

Alikulia katika kambi ya Khan Yunis, ambayo pia ilivamiwi wa Israeli mnamo 1967.

Al-Sanwar alipata elimu katika shule za kambi hiyo hadi alipomaliza masomo yake ya sekondari, kisha akajiunga na Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Gaza ili kukamilisha elimu yake ya chuo kikuu na kupata shahada ya kwanza katika lugha ya Kiarabu.

1982, alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa miezi minne kwa tuhuma za kujihusisha na "shughuli za uasi."

1988 mahakama ya Israel ilimhukumu Sinwar kifungo cha maisha jela mara nne (kipindi cha miaka 426), alikaa gerezani miaka 24.

Ushawishi wake

Sinwar anatajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika maeneo ya Palestina, kulingana na jarida la Uingereza la The Economist.

Alikuwa mmoja wa wanachama wa kwanza wa harakati ya Hamas. Alihusika kuundwa kwa timu ya usalama wa ndani, iitwayo Majd. Huhusika na masuala ya usalama wa ndani na kufualia mtandao wa ujasusi wa Israel.

Wakati Israeli ilipofanya mazungumzo ya kubadilishana wafungwa wa Kipalestina na mwanajeshi wake Gilad Shalit, ambaye alitekwa na Hamas mwaka 2011.

Israel ilimtumia Sinwar kama mpatanishi, kwa mujibu wa The Economist, alizungumza na viongozi wa Hamas ambao walitaka kuachiwa huru zaidi ya wafungwa 1,000 wa Kipalestina .

Israel ilipinga idadi ya majina yaliyopendekezwa na Hamas, na Sinwar hakuwa miongoni mwa wale waliopingwa. 2011, Al-Sinwar aliachiliwa na kuwa kiongozi katika Brigedi za Izz al-Din al-Qassam, jeshi la Hamas.

Al-Sinwar alinufaika na ujuzi wake wa magereza ya Israel, alioupata wakati akiwa kwenye kona za gereza kwa miaka mingi, jambo ambalo lilimpa ushawishi miongoni mwa uongozi wa kijeshi wa Hamas.

Katika ngazi ya kisiasa, mwaka 2017 Sinwar alichaguliwa kuwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati hiyo katika Ukanda wa Gaza.

Mwaka huo huo, alichukua nafasi kubwa ya kidiplomasia katika kujaribu kurekebisha uhusiano kati ya Mamlaka ya Palestina, inayoongozwa na harakati ya Fatah katika Ukingo wa Magharibi na harakati ya Hamas huko Gaza, lakini jaribio hili halikufaulu.

Sinwar pia alifanya kazi ya kutathmini upya uhusiano wa nje wa Hamas, ikiwa ni pamoja na kuboresha uhusiano na Misri.

Septemba 2015, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilimuweka Yahya Sinwar kwenye orodha ya magaidi wa kimataifa.


No comments