BILIONI 32 KUKARABATI, KUJENGA SOKO KUU KARIAKOO
 
SERIKALI imetenga shilingi bilioni 32.2 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa Soko jipya la kimataifa la Kariakoo ambalo linatarajiwa kujengwa hivi karibuni baada ya Rais Samia kusem fedha hizo tayari zimetengwa kwa ajili hiyo.
Jana Waziri wa TAMISEMI, Ummy
Mwalimu  alifika Kariakoo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa Soko
la zamani sambamba na ujenzi soko Jipya. "Nimefika leo kwa ajili ya
kufuatilia na kutekelezeka maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu
Soko la Kariakoo"
"Naelekeza Fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Tsh. Bil 32.2
ziombwe na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam sababu mradi huu ni mkubwa na
Wilaya watakua wafuatiliaji wa karibu lakini Mkoa lazima wasimamie kikamilifu,
ninachotaka kuona ni Soko lijengwe kwanza baadae ndo tutajua namna ya
Menejimenti kama lisimamiwe na Jiji au Shirika la Masoko Kariakoo" 
"Soko letu liliungua July, tulipeleka maombi kwa Mh.
Rais ya kulikarabati ametukubalia, na ametukubalia kujenga soko lingine kubwa
litakuwa na Ghorofa sita kwenda juu na mbili kwenda Chini” 
Ummy ameagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaam kuomba fedha
hizo Wizara ya Fedha na Mipango si zaidi ya November 15,2021 ili kazi ianze ———
"Soko Jipya litachukua wafanyabiashara zaidi ya elfu 2, kipaumbele
kitakuwa kwa wale waliokuwepo mwanzo, tunamshukuru Rais ametoa Bil. 32. 2
kukarabati soko la zamani bilioni 6 na kujenga soko jipya Bil. 26.2,
Wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi wote watapewa maeneo ya biashara"

 
Post a Comment